Breaking News

WAKULIMA KIDAZINI WADAI FIDIA

 ‎


Na Said Khamis.

Wakulima wanaofanya shughuli za kilimo katika eneo la shehia ya Kidazini wamewaomba wamiliki waliouza shamba ambalo hufanya shughuli za kilimo kuwalipa fidia ya vipando vyao walivyovipanda.

‎Wakizungumza na Ikhuan Media baadhi ya wakulima wamesema shamba hilo wameanza kufanya shughuli hizo muda mrefu lakini hivi sasa limeuzwa bila ya kupewa taarifa na wamiliki wa shamba.

‎Wameeleza kuwa awali shamba hilo lilikua ni pori lakini baadae wazee wao waliamua kupanda vipando vya muda mfupi kwa ajili ya kujipatia riziki.

‎"Hili eneo lilikua pori tupu kuna chatu na kima tu wazee wetu wakaamua kulilima hata hao wenyewe wahusika walikua hawalijui leo wameliuza washaanza kujenga kuta hata sisi wakulima hatujashirikishwa"

‎Akizungumzia kuhusiana na fidia ya wakulima hao mmoja wa waliokua wamiliki wa shamba hilo Seif Nassor maarufu Boka   amesema  wakulima wanatakiwa kumaliza kuvuna mazao yaliyobakia na sehemu iliyoharibiwa kwa ajili ya ujenzi wa uzio watalipwa na wamiliki walionunua.



‎" kuhusiana na malipo mimi sihusiki wenyewe walionunua ndio watakao walipa sisi hatuhusiki"

‎Nae sheha wa shehia ya Kidanzini Mzee Salmin Mbarouk amekiri kuwepo kwa mgogoro huo hivyo amewashauri wahusika kumtafuta mtathmini ili kuweza kuwalipa wakulima vipando vyao viliyoharibiwa katika ujenzi wa uzio.

‎Vipando vilivyoharibiwa katika ujenzi wa uzio huo nipamoja na mihogo,migomba,mihindi pamoja na mazao mengine


No comments