UVUVI, UTALII KUINUA ZANZIBAR KIUCHUMI
Na Said Khamis.
Mafanikio makubwa yamepatikana kupitia sekta za uchumi wa buluu na uvuvi kutokana na usimamizi mzuri wa hifadhi za bahari na rasilimali zake baharini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uhifadhi wa bahari Dkt. Makame Omar Makame kutoka Wazara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar amesema hayo huko Marumbi wakati wa uzinduzi wa Boti ya doria pamoja na makabidhiano ya Mashine ya boti hiyo.
Dkt. Makame amesema Sekta ya Mwani ,Uvuvi na Utalii zinachangia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi unaotokana na uhifadhi wa bahari hapa nchini.
Sambamba na hayo amesema kuwepo kwa boti ya doria kutaongeza jitihada za kusimamia matumizi bora ya bahari ili kuifanya Ghuba ya Chwaka kuimarika zaidi baharini.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Mwambao MCCC Dkt. Said Halid Said amesema Taasisi ya Mwambao ipo tayari kuisaidia Serikali kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za uhifadhi wa bahari kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla .
“Baada ya Wanamarumbi kutumia fedha zao za uhifadhi kuweza kununua boti ya doria hili jambo kubwa na kutufanya Wanamwambao kusaidia mashine ili boti hii iweze kufanya kazi iliyokusudiwa”.
Kwa upande wao Wavuvi wa Shehia ya Marumbi wamesema wastani wa asilimia 65% za wakaazi wa Marumbi wanafaidika na mazao ya baharini hivyo hakuna budi ya kuzisimamia na kuzilinda rasilimali za bahari.
Sambamba na hilo wametoa wito kwa Kamati jirani kuwa na mashirikiano ya pamoja juu ya suala zima la usimamizi wa eneo la Ghuba ya Chakwa MIMCA ili kudhibiti uvuvi haramu usiendelee kuathiri baharini.
“Kamati ya uvuvi ya marumbi inajishughulisha na ulinzi wa pamoja na utoaji wa elimu juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za bahari”
Jumla ya Shilingi milioni tisa (9) zimetumika kwa ajili ya ununzi wa Boti ya Doria fedha ambazo zimetoka Serikalini kupitia Kamati ya Usimamizi wa Hifdhi za bahari ya Marumbi pomoja na Shilingi Miloni nane (8) zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa Mashine ya Boti chini ya ufadhili wa Shirika la Mwambao MCCC ikiwa juhudi za kuungwa mkono Serikali ya awamu ya nane kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
No comments