MAMA WA MIAKA 67 AUWAWA NA KIJANA WAKE. MTONI ZANZIBAR.
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 67, Salama Abdallah Saidi, mkazi wa Mtoni, amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kisu nyumbani kwake, katika tukio lililoripotiwa Kituo cha Polisi Bububu mnamo Januari 7, 2026 saa 8:00 mchana.
mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mfanya kazi wa ndani wa Bisalama pamoja na jirani wameeleza kuwa chanzo cha tukio ni mgogoro wa kifamilia amabpo Wakati wa tukio, marehemu alikuwa nyumbani pamoja na mume wake, Ali Suleimani (75), ambaye ni mgonjwa na huhitaji msaada wa karibu kutokana na hali yake ya afya. Inadaiwa kuwa marehemu alimwomba mtuhumiwa amsaidie baba yake, jambo lililopingwa na mtuhumiwa na kuibua mzozo uliosababisha shambulio hilo.
Baada ya kushambuliwa, marehemu alipoteza damu nyingi na alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya KMKM Kibweni. Mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Lumbumba kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu (postmortem).
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtoni, Shehia ya Mtoni, Wilaya ya Magharibi “A”, Mkoa wa Mjini Magharibi. Marehemu alishambuliwa akiwa mlangoni mwa nyumba yake namba MT.88. Anayedaiwa kutekeleza shambulio hilo ni Ibrahim Ali Suleimani (39), mkazi wa Mwanyanya, ambaye ni mtoto wa kumzaa wa marehemu.
kwa mujibu wa ASP Ambokile, mbinu iliyotumika kufanya mauwaji hayo ni kuvizia na kumjeruhi marehemu kwa kisu, hali iliyomzuia kuomba msaada kwa majirani au mfanyakazi wa ndani aliyeshuhudia tukio. Mtuhumiwa alikimbia eneo la tukio mara baada ya shambulio, lakini amekamatwa na kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Bububu kwa mahojiano na hatua zaidi za kisheria.
Akizungumza na Ikhuan Media Sheha wa Mtoni, Sahra Hassan Mohammed, amesema alipata taarifa hiyo kutoka kituo cha polisi mtoni, ndipo alipofuatilia na kugundua kuwa chanzo kikubwa cha mmauaji hayo ni mgogoro wa kifamilia.
kwa sasa kesi hiyo ipo kituo cha polisi kwa hatua za uchunguzi.

No comments