ZANZIBAR YAJIKITA KATIKA TAKWIMU SAHIHI NA MIUNDOMBINU YA KISASA KUINUA UCHUMI WA WAVUVI
Na Said Khamis.
Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga amesema Serikali ya awamu ya nane imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya uvuvi ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya uvuvi ya kisasa ,Kuanzishwa kwa Chuo cha uvuvi pamoja na kuimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari kwa lengo la kukuza ajira nchini.
Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku ya Mvuvi Duniani lililofanyika ukumbi wa Ziwani Polisi lenye Kauli Mbiu ya “Tuimarishe Biashara ya Mazao ya Baharini kwa Kutumia Takwimu Sahihi za uvuvi ili Kuinua Kipato cha Wavuvi”.
Mhe. Mboja amesema Serikali kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi inafanya juhudi kubwa ya kufanya mkakati wa mageuzi ya kujenga bandari za uvuvi ,Madiko na Masoko ya kisasa ,mifumo ya baridi pamoja na usindikaji wa dagaa na mwani ili kuwasaidia Wavuvi kuinua uchumi wa mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
“Lengo la mikakati hii ni kuongeza wataalamu katika sekta ya uvuvi pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya baharini pamoja na kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na kuwawezesha wavuvi wadogo wadogo wakiwemo wanawake kupitia fursa za uchumi wa buluuhii yote ni juhudi za Mhe. Rais wa Zanzibar kuwawezesha Wavuvi kuinua kipato cha maisha yao ili kuacha na athari zinazofanyika baharini”
Sambamba na hayo ametoa wito kwa Jamii kutoa mashirikiano na Taasisi husika juu ya usimamizi wa rasilimali za bahari nchini kutokana na zaidi ya watalii laki nane mwaka jana wamevutiwa na maeneo ya hifadhi za bahari ya Zanzibar jambo ambalo limeleta faraja kubwa kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.
“Uvuvi haramu bado changamoto kubwa unaoathiri rasilimali zetu kuongeza harama za doria pamoja na kupunguza upatikanaji wa takwimu sahihi za Serikali “
Aidha amesema Serikali kupitia Taasisi husika imeandaa utaratibu wa kusajili wavuvi katika mfumo maalum wa kupatiwa vitambulisho vya kisasa pamoja na uoatikanaji wa huduma za bima na mikopo kwa wavuvi ili kupunguza wimbi la uharibifu wa rasilimali za bahari.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Keptain Hamad Bakari Hamad amesema lengo la kuwepo kwa sherehe ya mvuvi ni kuwa pamoja kwa ajili ya kutathmini na kutatua changamoto zilizopo na namna gani zinaweza kutatulika kwa maslahi ya wavuvi na Serikali kwa ujumla.
Keptein Hamad amesema Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi imeweka kipao mbele sekta ya uvuvi kwa lengo la kuinua kipato cha wavuvi wadogo wadogo kitachotokana na uchumi wa buluu hapa nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uhifadhi wa Bahari Zanzibar Dkt. Makame Omar Makame amesema wavuvi wadogo wadogo nchini wanamchango mkubwa katika sekta ya uvuvi kutokana na idadi kubwa ya jamii wa ukanda wa pwani wamejiajiri na shughuli za baharini na kuleta mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya uvuvi.
Dkt. Makame amesema kupitia Kongamano hili la Mvuvi Takwimu za uvuvi ni muhimu kwa sababu zinasaidia kutambulika katika uzalishaji wa mazao ya baharini ,kujua idadi ya wavuvi pamoja na kupata takwimu sahihi za usafirishaji wa mazao ya baharini ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika WorldFish Dkt. Paskal amesema Serikali kwa kushirikiana na Shirika la World Fish limeboresha mifumo ya ukusanyaji wa taariza za uvuvi katika maeneo ya Zanzibar kwa lengo la upatikaniji wa takwimu sahihi na kwa wakati uliokusudiwa.
Kwa upande wao Wawasilishaji wa Mada za Uvuvi Nd. Maryam Ramadhan Mwinyi kutoka idara ya Uhifadhi wa Bahari amewataka Wavuvi kutumia fursa hii ya siku ya mvuvi kuwa mabalozi wa kufikisha taaluma iliotolewa kuipeleka kwa jamii ili kuisaidia Serikali juu ya kuzilinda rasilimali za bahari kwa maslahi ya sasa na baadae.
Jamila Haji Taasisi ya Utafiti ZAFIRI ametoa wito kwa Wavuvi kuendelea kuyatunza maeneo ya hifadhi ya Chwaka , Kisiwa Kwale na Kisiwani Bawe kutokana na kuonesha majibu ya utafiti wa Nyasi bahari na Matumbawe kwa kiasi kikubwa yameimarika baharini.
Nae Ali Khamis Shafi kutoka Idara ya Maendeleo ya Uvuvi amesema Serikali kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ipo mbioni kujenga Viwanda vitatu chini ya ufadhili wa Shirika la IFAD kiwanda chengine kikubwa kitajengwa kupitia mradi wa TASFAM kwa ajili ya kusari zao la mwani ili kukuza uchumi unaotokana na zao hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Wakulima wa mwa ni Nd. Semen Mohd Salum kutoka Ushirika wa Wakulima Hai amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwashirikisha Siku ya Mvuvi na kuwaletea mfumo wa uchukuaji wa takwimu za uzalishaji wa mwani jambo ambalo limeleta faraja kwa wakulima ili kupatikana data kwa wakati za uzalishaji wa zao la hilo. Kongamano hilo limefanyika kwa mashirikiano ya Wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi.WorldFish .CGIAR .ZAFIRI na Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.




No comments