WATENDAJI WA WIZARA YA ARDHI WAPATIWA MAFUNZO YA KUJIKINGA NA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI
Na Said Khamis.
Watendaji wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi wamepatiwa mafunzo kuhusu kuzuia vitendo vya rushwa, uhujumu uchumi, pamoja na kufuata sheria na kanuni za utumishi wa umma katika maeneo yao ya kazi.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo katika ukumbi wa wizara Maisara, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi, Khamisuu Hamid Mohammed, aliwataka watendaji hao kuyafanyia kazi mafunzo waliyopata ili kuongeza ubunifu, ufanisi na kuboresha huduma kwa jamii.
Naye Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), Yussuf Juma Slim, aliwahimiza watumishi wa umma kushirikiana na mamlaka hiyo katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi.
Aidha, aliwataka watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa umma ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya kukuza utawala bora nchini.
Kwa upande wake, Afisa kutoka Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Khadija Mohamed Saleh, aliwasisitiza watumishi kufanya kazi kwa bidii na kutumia haki na taratibu zilizopo ili waweze kupata haki zao za kiutumishi bila usumbufu.


.jpeg)
No comments