WANACHI WAASWA KUZITUNZA BARABARA.
Na Siti Ali.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Anna Athanas Paul amewataka wananchi kutunza na kuzilinda babarabra zinazojengwa na serikali ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kuacha kupitisha magari yenye uzito mkubwa katika maeneo yasioruhusuwa kisheria
Aliyasema.hayo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Mwakaje (Selemu_Mbuzini yenye ukubwa wa km 3.5. Ikiwa ni yenye thamani ya shilingi bilioni 3.8ch8ni ya wasimamizi ecocity building material ikiwa ni shamrashamra za kuelekea miaka maoinguzi zanzibar
Amesema kuw hatua hiyo iendane sambamba na kuzingatia sheria za usalama.barabarani kwa kutoharibu kwa kungoa alama zilizowekwa katika barabara hiyo na kuwataka kutoa taarifa pale panapojitokeza vitendo vya uharibifu ili wachukuliwe hatua za sheria.
Aidha lisema barabara hiyo imetumia jumla ya shilingi 305,052,110 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi wapatao 40 ambao vipando vyao viliathirika katika ujenzi wa barabara hiyo.
Hata hivyo Waziri huyo alisema kuwa serikali inatambua kuwa wapo baadhi ya wananchi hawajalipwa fidia za vipando vyao lakini wasubiri kwani hatua zinaendelea.
Akizungumzia miongoni mwa mafanikio yatakayopatikana kupitia ujenzi huo alisema wakulima na wafanyabiashara wataongeza uzalishaji kutokana na ongezeko la masoko na gharama za usafiri kupungua kufuatia miundombinu hiyo.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Bakari Said aliwataka wananchi waliolipwa fidia katika barabara hiyo kutokurudi katika maeneo ya hifadhi ya barabara huku akiahidi kuondosha wafanyabiashara wote wanaotumia maeneo ya hifadhi.
Hata hivyo alisema serikali haitomvumilia mwananchi yoyote ambae atavamia ama kuyatumia maeneo hayo huku akihimiza umuhimu wa watu kuheshimu na kufuata sheria.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara Zanzibar Mhandizi Cosmas Masolwa alisema ujenzi wa barabara hiyo imetatua shida za wananchi na itarahisisha usafiri na usafirishaji wa wananchi na bidhaa zao.
Aliongeza kuwa ni miongoni mwa barabara za ndani zilizokuwa zikilalamikiwa na wananchi kutokana na ubovuwake.
Alifahamisha kuwa barabara hiyo inaunganisha barabara kuu ya Mfenesini, Mwera,,Soko la Chuini na Mkanyageni na imejengwa kwa kiwango cha lami kilichozingatia ubora wa viwango.
Aidha alisema mradi huo umegharamiwa na serikali na kusimamiwa na Wakala wa Barabara Zanzibar.

No comments