Breaking News

WAZIRI RAHMA AWATAKA WATENDAJI KUONGEZA KASI YA HUDUMA.



Na said khamis.

‎Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Rahma Kassim Ali amewasisitiza Watendaji wa Wizara hiyo kuongeza kasi ya utendaji katika kuwahudumia wananchi kwa kulingana na mahitajia katika utoaji wa huduma zake.

‎Mhe. Rahma ameyasema hayo alipokua akizungumza na wafanyakazi hao huko katika ukumbi wa Wizara hiyo maisara Mkoa wa Mjini Magharibi.

‎Aidha amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwneyeketi wa Baraza la Mapinduzi kwa kumuamini tena pamoja na kuwapongeza Wafanyakazi hao kutokana na mashirikiano waliyomuonesha katika kipindi kilochopita cha kuiongoza Wizara hiyo sambamba na kuridhika na mwendeno wa kazi zinazotekelezwa na Wizara.

‎Hata hivyo amewataka wafanyakazi hao kuendeleza mashirikiano ya pamoja ambayo ndiyo nguzo itakayoweza kuleta mafanikio zaidi na kuipatia sifa taasisi hiyo.

‎Akizungumzia kuhusiana na utendaji kazi Mhe.Rahma amewataka Watendaji hao kua na lugha nzuri katika utoaji wa huduma kwa wananchi wanaofika katika taasisi hiyo pamoja na kudhibiti siri za ofisini.

‎Mapema Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mh.Salha Mohammed Mwinyjuma amesema Taasisi ni kiungo Muhimu cha kuipelekea Zanzibar katika Mabadiliko ya mafanikio katika utoaji wa huduma kwa Jamii.



‎Akizungumza kwa niaba ya Watendaji Mkuruegenzi Mipango Sera na Utafiti Makame Salum Ali ameahidi kuendeleza mashirikiano hayo kama ilivyokua katika kipindi kilichopita kwa ili kuweza kutimiza malengo ya liyokusudiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara hiyo




No comments