Breaking News

LESENI 73 ZA MADINI AMBAZO HAZIJAENDELEZWA ZAFUTWA

 


▪️Ni Leseni za Utafiti na Uchimbaji Madini wa Kati.

▪️Ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia  kuwezesha Vijana 

■ Waziri Mavunde aelekeza zielekezwe kwenye Programu ya MBT na wawekezaji walio tayari

■ Eneo la ekari 741,494 lilihodhiwa bila kufanyiwa kazi


DODOMA

WAZIRI wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde ameilekeza Tume ya Madini kufuta leseni 73 za uchimbaji wa kati na utafiti wa madini ambazo hazijaendelezwa.

Mhe. Mavunde ametoa maelekezo hayo leo Novemba 25, 2025 wakati akiongea na vyombo ya habari katika ukumbi wa Ofisi za Tume ya Madini mjini Dodoma.

Mhe. Mavunde amesema kuwa , ufutaji wa leseni hizo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuiwezesha Wizara ya Madini kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa na kuhakikisha rasilimali  madini zinawanufaishaWatanzania na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Mavunde ameongeza kuwa, eneo lenye ukubwa wa ekari 741,494 lilihodhiwa bila kufanyiwa uendelezaji wowote , jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Madini , Sura 123.
  
Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Leseni zilizofutwa ni pamoja na leseni za utafutaji wa madini 44   na leseni 29 za uchimbaji wa Kati kutokana na  kushindwa kurekebisha makosa yao.

Akielezea kuhusu matumizi ya maeneo yote yaliyofutwa, Mhe. Mavunde amesema kuwa, maeneo hayo yatapangwa kwa ajili ya mradi wa vijana katika programu ya Mining Better Tomorrow (MBT) ili waweze kunufaika na rasilimali madini.



No comments