Breaking News

WAFANYA BIASHARA DUMISHENI USAFI, KUEPUKA MARADHI.''AMOUR BADALI''



Na Said khamis

Wafanyabiashara wametakiwa kufahamu wajibu wao wakuyatunza na kuyahifadhi mazingira katika maeneo yao ya kufanyiabiashara ili kuepukana na maradhi mbalimbali.

‎Hayo ameyasema Mkuu wa Divisheni ya Mazingira wa Manispaa Kati Amour Badali Amour wakati wakitoa elimu ya usafi na utunzaji pamoja na kuwataka wafanyabiashara kueka taka  maeneo rasmin yaliyotengwa na baraza hilo. mazingira kwa wafanyabiashara wa shehia ya Jumbi na Tunguu huko katika skuli ya Jumbi msingi Wilaya ya Kati.

‎Amesema wafanyabiashara wanatakiwa kufuhamu wajibu wao katika suala zima la usafi hususani katika maeneo yao ya biashara na maeneo yaliyowazunguka ili kupambana na adui maradhi anaeweza kuleta athari katika jamii.

‎‎"Sheria zipo zimeekwa maalum zinazoelekeza nani mwenye wajibu wa kutunza mazingira, nani msimamizi wamazingira na kunaathari gani zinazoweza kujitokeza kwa mtu anaekiuka hizo taratibu " Alisema Amour



‎Kwa upande wake sheha wa shehia ya Jumbi Muhidini Haji Machano ameeleza kuwa suala la usafi si la mtu mmoja pekee bali ni jambo la mashirikiano baina ya manispaa na jamii kwani jukumu la usafi na utunzaji wa mazingira ni lakila mwananchi.

‎"Usafi ni afya kila mwananchi anajukumu la kusafisha na kutunza mazingira katika makaazi yao yanayowazunguka" alisema Sheha

‎Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Usafi Haji Mohammed Iddi ameliomba baraza la manispaa kati kuchukua taka kwa wakati  ili maeneo yakufanyiabiashara yaweze kuwa safi na salama muda wote.

‎Aliongeza kusema kuwa watahamasisha wafanyabiashara kueka taka hizo maeneo rasmin yaliyotengwa na manispaa ilikuepuka kuzagaa kwa taka mitaani.

‎Hata hivyo Mwenyekiti huyo ameendelea kuliomba baraza hilo kutoyaharusu magari yakusafirishia taka kutembea muda wa mchana kwani yanaleta kero kwa wananchi kutokana na harufu kali.



‎" Magari yanatoka Mjini yamebeba taka yanakua yanaharufu wananchi wanaoishi karibu na barabara hukirihishwa na hali hiyo bora yatembee muda wausiku wananchi wengi watakua wamelala" alisema Mwenyekiti

‎Akizungumza kwaniaba ya wafanyabiashara wenzake Asia Habibu amesema kwa upande wao wanakabiliwa na changamoto ya kuchelewa kuchukuliwa taka zao katika maeneo ya kufanyiabiashara hali inayoweza kuhatarisha usalama wa afya zao.

‎Zaidi ya Wafanyabiashara 50  wa Shehia ya Jumbi na Tunguu  wamepatiwa elimu, ufafanuzi na maelekezo ya Usafi na utunzaji wa Mazingira ili kupambana na adui uchafu katika maeneo ya kufanyia Biashara.


2 comments:

  1. ni wajibu kutunza mazingira, na kudumisha usafi hasa kipindi hiki cha mvua

    ReplyDelete